LIVERPOOL NA HATIHATI YA KUONDOLEWA KWENYE KOMBE LA LIGI:s
Liverpool ipo kwenye hatihati ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) ikiwa itabainika walimchezesha mchezaji ambaye hakuwa na sifa za kucheza kwenye mechi ya juzi Jumatano dhidi ya MK Dons kwenye ushindi wa 2-0 kwenye michuano hiyo. Liverpool inachunguzwa na wasimamizi wa michuano hiyo (EFL) kufuatia madai kuwa ilimchezesha mchezaji ambaye hakuwa amekidhi vigezo vya kushiriki kwenye michuano hiyo. Kwa maana hiyo wako hatarini kufutwa kwenye kombe hilo kabla hata ya pambano lao dhidi ya Arsenal mwezi ujao kwenye kombe hilo ikiwa mchezaji huyo ambaye mpaka sasa jina lake halijatajwa itabainika hakukidhi vigezo. Msemaji wa Liverpool amesema: "Klabu inafahamu suala la kiutawala kuhusiana na mmoja wa wachezaji wetu". "Tunashirikiana na mamlaka husika ili kutafuta ukweli wa jambo hilo na hatutatoa majibu yoyote mpaka mchakato huu ukamilike". Msemaji wa EFL, amesema; "Kwa sasa tunalishughurikia hili suala". Kama watakutwa na hatia basi EFL w...