Posts

Showing posts from July, 2019
Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids? Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye uterus. Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa. Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji. Chanzo Cha Fibroids Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kuku...