Chaneza Waanzisha mashindano mapya ili kuupa hamasa mchezo huo.
Mashindano ya mpira wa pete kwa kuadhimisha moaka 55ya mapindizi ya Zanzibar yanatarajiwa kukata utepe hapo kesho katika uwanja wa jimkana saa kumi za jioni timu nane za kike zitashiriki mashindano hayo. Akiongea na kipindi hiki katibu mkuu wa chama cha mpira wa pete zanzibar Saidi Ali Mansab amesema maandalizi kwa upande wao yamekamilika na kinachosubiriwa ni wakati na filimbi kupuulizwa. Amesema mashindano hayo yamepewa baraka na kamati ya sherehe na mapambo kwa kuwawezesha chama cha Netbal kuandaa mashindano hayo Mashindano ya Mapinduzi Cup kwa netball ni ya kwanza kufanyika hapa Zanzibar na kwa mujibu wa katibu wa chaneza amesema wanatarajia kuwa endelevu ili kila mwaka yaweze kufanyika kwani wana malengo makubwa ya baadae.