Posts

Showing posts from November, 2017
Image
FORO FORO FURAHA AU MISIBA? NA : HAMAI VUAI USSI Kama ambavyo wageni (sikusudii wa Bara) wanapo ingia Zanzibar aghalab hukusudia kuutembelea (mji mkongwe, sehemu za makumbusho hata za mashamba, kuona hali ya maisha ya watu kiujumla), na mwishowe kujimwaga Foro. Wageni wa nchi jirani wanapo ingia Z'bar, pia nao hukusudia matembezi ya sehemu za mji wa Zanzibar, na hatimae ni Foro. Amma sisi wenyewe Wazenj, kilele cha furaha yetu kuishi Z'bar, ni kuwepo Forodhani, kukoga, kutembea, kupiga soga, pia ndio meeting point ya wengi. Zanzibar bila ya Foro haipo. Tokea hapo kale, kukoga Forodhani au kujifundisha kukoga kwa styles zote huanzia au huishia hapo, Generation kwa generations. Kama ni hivo, Jee, municipal au serikali kwa jumla, imewahi kufikiria umuhimu wa eneo wanalokoga vijana wetu (usalama wake na unadhifu wake)? Jee hii sehemu muhimu ya bahari ambayo ni ukingo wa MAWE na ufukwe wa mawe - kokoto na machupa, tuseme serikali haioni au anatafutwa Mfadhili k