Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, amewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kukuza na kulea vipaji vya wanafunzi. Hayo ameyaeleza wakati akifunga Tamasha la tatu la Michezo la Skuli ya Leera la mwaka 2024 lililofanyika kwenye uwanja wa Amani Complex . Alisema watoto hao watakapoekewa mashirikiano baina pande zone mbili watakuja peperusha bendera ya Taifa katika kuimarisha michezo. Aliwataka skuli ya Leera kuendelea kuibua vipaji kwani miundo mbinu ya michezo inaendelea kukua kwa kasi zaidi pia ni vyema kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa jitihada za kuimarisha sekta ya Michezo nchini. Waziri Tabia alieleza Serikali imetenga fedha billion 70 katika sekta ya michezo, hivyo hawanabudi kuthamini michezo na kuiendeleza katika skuli kwa watoto wao. Akisoma risala ya Skuli hiyo Mkuu wa Utawala Jonathan Kahatano, alisema skuli hiyo inatoa taaluma bora ikiambatana ...